Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Ujenzi

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI

Habari

​Waziri Simbachawene azindua Wiki ya Utumishi wa Umma


image title here


  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amezindua Wiki ya Utumishi wa Umma na kusisitiza matumizi ya TEHAMA.

Mhe. Waziri amefanya uzinduzi huo jijini Dodoma, katika viwanja vya Chinangali Park, ambapo Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limeshiriki kwa kuweka banda lake, ili kuhudumia wananchi na kujitangaza.

Katika hotuba yake, Waziri Simbachawene amesema TEHAMA inayohusisha mifumo ya kidijiti inarahisisha utoaji taarifa na kuchochea uwazi katika utoaji huduma. Amezitaka taasisi zote za umma kutumia mifumo ya kidijiti.

Katika kuonesha kuwa inatambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya kidijiti kama Waziri Simbachawene anavyosisitiza, NCC imetengeneza mfumo wa makadirio ya gharama za ujenzi (Construction Cost Estimation System) unaowezesha kuwepo kwa bei elekezi za ujenzi na kusaidia kudhibiti bei, pamoja na gharama za ujenzi.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yatahitimishwa tarehe 23 Juni, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, NCC imeendelea kuhudumia wananchi waliotembelea banda lake, na itaendelea kufanya hivyo kufikia kilele cha wiki hiyo.