MAFANIKIO YETU
1. Kaguzi za Kiufundi
Baraza limefanya kaguzi mbalimbali za kiufundi kwa miradi ya ujenzi nchini ikiwemo ya barabara na majengo.
2. Huduma za Ushauri
Baraza limekuwa likitoa huduma mbalimbali za ushauri.
3. Madai ya Ujenzi
Katika eneo la madai katika ujenzi, Baraza limesaidia taasisi zifuatazo katika uchambuzi wa hasara na gharama za wakandarasi zikiwemo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
4. Maandalizi ya gharama za ujenzi wa barabara
Baraza kwa kushirikiana na Bodi ya Mfuko wa Barabara wameandaa viwango vya gharama za ujenzi wa barabara. Katika utekeleza kazi hiyo, Baraza limefanikwa kuanzisha mfumo wa viwango vya gharama za barabara kulingana na viwango msawazo vya barabara ya mwaka 2000 vya Wizara ya Ujenzi na viwango vya matengenezo ya mwaka 2010.
Baraza lilianzisha viwango hivyo kutokana na kanuni halisia. Uzalishaji wa viwango kwa kutumia kanuni halisia ni msingi katika makadirio ya gharama halisi katika ujenzi wa barabara tofauti na njia ya awali ya makadirio kwa misingi ya takwimu za kihistoria.
Hivyo, uzalishaji wa viwango hivi utasaidia watumiaji katika tasnia ya ujenzi kuandaa gharama halisi za miradi ya barabara kwa takwimu za sasa na kuleta thamani ya pesa.
Baraza limekuwa likishiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali ya kitaifa yakiwemo:
5. Uratibu wa Utatuzi wa Migogoro
Rejista ya Waamuzi na Waamuzi Walioidhinishwa:
Baraza linaendelea kutunza rejista ya Waamuzi na Wasuluhishi walioidhinishwa.
Uratibu wa Utatuzi wa Migogoro:
Baraza limekuwa likiratibu utatuzi wa migogoro katika sekta ya ujenzi. Uratibu huu umewezesha utatuzi wa haraka wa migogoro, hivyo basi kuokoa muda na gharama.
6. Mafunzo
NCC imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali yanayohusu sekta ya ujenzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau kutoka Taasisi za Serikalini na binafsi. Mafunzo yamesaidia utendaji wa washiriki katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Vile vile, takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya washiriki inaongezeka kutokana na umuhimu wa mafunzo yanayotolewa na Baraza.
7. Fahirisi za Gharama za Ujenzi
Tangu 1990 Baraza limekuwa likizalisha fahirisi za gharama za rasilimali watu na vifaa vya ujenzi. Fahirisi hizi hulenga kufuatilia mabadiliko ya mara kwa mara ya bei za vifaa pamoja na malipo ya rasilimali watu katika miradi ya ujenzi. Baraza huandaa na kutunza taarifa za kila mwezi za gharama za rasilimali watu, Nondo, Mafuta, Mbao Ngumu, Mbao Laini, Kokoto, Saruji, Rangi, Chuma ‘Z’ Purlin, Mabomba ya Mabati