Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Ujenzi

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI

Eneo


Picha
Taarifa

UTAFITI

Kazi za utafiti zinazolenga katika kutambua matatizo mbalimbali na ufumbuzi wake yanayohusiana na sekta ya ujenzi kwa ujumla, ni mojawapo ya shughuli za Baraza. Tafiti zilizowahi kufanywa na Baraza ni pamoja na:

1. Tafiti kuhusu uanzishwaji wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadau wa sekta ya ujenzi kupata mahali pa kukopa fedha au kupata dhamana kwa ajili ya miradi ya ujenzi;

2. Mahitaji ya mafunzo kwa washauri elekezi wazawa katika uhandisi wa barabara;

3. Mahitaji ya rasilimali watu katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania;

4. Mahitaji ya mafunzo kwa washauri na wakandarasi wa miundombinu ya umwagiliaji katika kilimo;

5. Uanzishwaji wa mfuko endelevu wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi nchini;

6. Mapendekezo ya kuhuishwa sheria iliyoanzisha Baraza la Taifa la Ujenzi;

7. Utafiti kuhusu namna ya kuliwezesha kifedha, Baraza la Taifa la Ujenzi ili kuweza kutekeleza majukumu yake;

8. Utafiti kuhusu ajira katika miradi mikubwa nchini;

9. Mapitio ya kitaasisi na kisheria kutoka kuhusu ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi nchini;

Utafiti kuhusu wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi katika ujenzi