Mafunzo yatolewayo na baraza yanalenga kuboresha uwezo na utendaji wa watendaji katika Sekta ya Ujenzi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Mafunzo hayo husaidia katika upatikanaji wa mbinu bora zinazohitajika katika uboreshaji wa huduma, hivyo kuimarisha ushindani na kuhakikisha thamani ya pesa kwenye miradi inayojengwa.
Baraza linaendelea kutekeleza mipango kadhaa ya mafunzo kwa vitendo. Maeneo mahususi yanayozingatiwa ni pamoja na: Manunuzi ya Umma, Usimamizi wa Mikataba na Miradi ya Ujenzi, Makadirio ya Gharama za Ujenzi, Kaguzi za Kiufundi, Usuluhishi wa Migogoro katika utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (Usuluhisi nje ya Mahakama), Madai katika Miradi ya Ujenzi, Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Teknolojia ya nguvu kazi katika ukarabati wa Barabara, Ukarabati wa Majengo.
Baraza pia huendesha mafunzo kulingana na huitaji wa wateja.
Mafunzo yatolewayo na Baraza hulenga washiriki kutoka fani mbalimbali zikiwemo: Wahandisi, Wasanifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Wathamini, Wasimamizi wa Majengo, Wataalamu wa Bima, Wahasibu, Wanasheria, Wakadiriaji Vipimo, Maafisa Ununuzi na Ugavi, Maafisa Mipango, Washauri Elekezi na Mafundi.
MAFUNZO TUNAYOTOA
- Usimamizi wa Mikataba ya Ujenzi
- Usimamizi wa Madai na Migogoro katika Ujenzi
- Marekebisho ya Bei katika Miradi ya Ujenzi
- Utatuzi Mbadala wa Migogoro katika Ujenzi kupitia Uzoefu wa pamoja.
- Usuluhishi katika mikataba ya Ujenzi
- Usimamizi wa mikataba ya ubunifu na ujenzi
- Manunuzi katika Mikataba ya Ujenzi
- Makadirio ya Gharama za Mradi kwa kazi za Barabara
1. MIKATABA YA JENGA SANIFU
Malengo ya mafunzo
Mafunzo haya yanawapa washiriki ujuzi juu ya kanuni za kusanifu na Kujenga;manunuzi ya huduma za Sanifu Jenga, mikataba ya huduma ya Sanifu Jenga, Utekelezaji na ukamilishaji wa Miradi ya Sanifu-Jenga, Usuluhishi wa migogoro, Changamoto zinazoonekana kwa miradi inayotekelezwa chini ya usanifu na ujenzi na kuhakikisha kuwa changamoto zinamalizika au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Mada:
- Kanuni za Sanifu Jenga
- Mahitaji ya mradi na usanifu wa awali
- Wajibu wa Mwajiri
- Wajibu wa Mkandarasi
- Timu ya Usanifu na Ujenzi ya mkandarasi.
- Wajibu wa kuzaingatia katika usanifu jenga kuendana na mahitaji yaliyoainishwa katika mradi.
- Wajibu wa Usanifu wa Mkandarasi
- Dhamana na ukomo wake katika usanifu
- Kushughulikia changamoto za usanifu za Mkandarasi
- Majanga na Fidia za Bima
- Changamoto za sanifu jenga
- njia za kupunguza changamoto za sanifu jenga
Muda: Siku 5
2. NJIA ZA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA GHARAMA KATIKA MIKATABA YA UJENZI
Lengo la Mafunzo
Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi wa kukabiliana na mabadiliko ya gharama katika mikataba ya ujenzi.
Mada:
- Mikataba ya ujenzi
- Aina za mikataba ya ujenzi
- Usimamizi wa Mikataba ya ujenzi
- Umuhimu wa kuwepo kwa vipengele vya mabadiliko ya bei katika mikataba ya ujenzi
- Aina ya vipengele vya mabadiliko ya bei katika mikataba ya ujenzi iliyoandaliwa na - PPRA, NCC, FIDIC
- Matumizi ya vipengele vya mabadiliko ya bei katika mikataba ya ujenzi iliyoandaliwa na NCC
- Matumizi ya vipengele vya mabadiliko ya bei katika mikataba ya ujenzi iliyoandaliwa na PPRA/FIDIC
- Changamoto zinazojitokeza katika mikataba inayoruhusu mabadiliko ya bei.
- Njia za kukabiliana na changamoto za Mikataba inayoruhusu mabadiliko ya bei
Muda: Siku 5
3. USULUHISHI WA MIGOGORO KATIKA MIKATABA YA UJENZI
Lengo la mafunzo:
Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi na maarifa kwa njia ya vitendo juu ya utatuzi wa migogoro katika mikataba ya ujenzi kwa njia ya usuluhishi na njia nyingine mbadala (ADR).
Mada
- Njia tofauti za usuluhisi wa migogoro ya ujenzi
- Usuluhishi katika Mahakama
- Sheria ya Usuluhishi Tanzania,
- Uteuzi wa Wasuluhishi,
- Madaraka na Mamlaka ya Msuluhishi,
- Maombi na uamuzi katika Usuluhishi,
- Taratibu za usikilizaji,
- Gharama na riba,
- Tuzo na taratibu za kukata rufaa,
- Mtihani kwa washiriki wanaotarajia kujiunga na Jopo la Wasuluhishi la NCC.
Muda: Siku 3
4. USIMAMIZI WA MABADILIKO YA KAZI, MADAI NA MIGOGORO
Lengo la mafunzo:
Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi unaohitajika katika kusimamia mabadiliko ya kazi jinsi ya kusimamia madai na migogoro katika miradi ya ujenzi.
Mada:
- Utangulizi kuhusu mabadiliko katika kazi za ujenzi
- Tathmini ya athari za mabadiliko katika kazi za ujenzi
- Taratibu za kuthaminisha mabadiliko katika kazi za ujenzi na Udhibiti wa mabadiliko ya gharama
- Njia mathubuti za jinsi ya kusimamia mabadiliko ya kazi .
- Aina za Madai
- Taratibu za kuandaa madai
- Uchambuzi wa Madai
- Taratibu za usimamizi wa madai
- Mbinu za Kupunguza Madai
- Utatuzi wa Migogoro katika Miradi ya Ujenzi
- Mbinu tofauti za utatuzi wa migogoro
- Uamuzi katika Mkataba wa Ujenzi
- Usuluhishi katika Mkataba wa Ujenzi
- Kusimamia Migogoro ya Ujenzi
- Mifano hai juu ya mabadiliko ya kazi na madai
- Mifano hai juu ya Utatuzi wa Migogoro
Muda: Siku 5
5. USIMAMIZI WA MKATABA YA UJENZI
Lengo la Mafunzo:
Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi wa usimamizi bora wa mikataba ya ujenzi.
Mada:
- Usimamizi wa Awali kabla ya uingiwaji wa Mkataba
- Utayarishaji wa mikataba
- Haki na wajibu wa wahusika katika mkataba
- Jinsi za kuzuia viatarishi katika miradi ya ujenzi
- Dhana ya Usimamizi wa Miradi
- Usimamizi wa ubora na udhibiti wa gharama
- Kufungwa kwa mkataba
- Mbinu za usimamizi wa madai na utatuzi wa Migogoro
- Mifano hai
Muda: Siku 5
6. MAKADIRIO YA KAZI ZA UJENZI WA BARABARA
Lengo la Mafunzo:
Mafunzo haya yatawapa washiriki ujuzi wa maandalizi bora ya gharama za ujenzi wa Barabara
Mada:
- Mipango ya awali ya mkataba
- Uchunguzi wa awali wa hali ya barabara
- Ufafanuzi na utayarishaji wa makadirio ya bei ya ujenzi wa Barabara
- Uandaaji wa gharama za ujenzi
- Uandaaji wa bajeti
- Uandaaji wa Mpango kazi na ripoti kwa kutumia tehama
- Mfano hai kuhusu makadirio ya kazi za ujenzi wa Barabara
7. USIMAMIZI WA UNUNUZI KWA MIKATABA YA UJENZI
Lengo la mafunzo:
Mafunzo haya yatawapa washiriki kuelewa mifumo ya kisheria, kanuni na taratibu za manunuzi katika miradi ya ujenzi.
Mada:
- Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya 2023 na kanuni zake
- Kanuni na taratibu za utoaji wa zabuni kwa kazi za ujenzi
- Maandalizi ya Zabuni,
- Tafsiri ya masharti na vigezo vya zabuni pamoja na tafsiri ya taarifa za kifedha,
- Tathmini ya zabuni
- Majadiliano ya awali ya kimkataba.
Muda: Siku 5