Huduma za Miliki
Huduma za Miliki
Imewekwa: 12 September, 2024
Kurugenzi ya Usimamizi wa Miliki inatoa huduma zifuatazo:
- Kutoa ushauri kuhusu usimamizi wa Miliki za Serikali, kutwaa na kuendeleza ardhi, uundaji wa sera mbalimbali za ndani za makazi ya Serikali, kanuni na taratibu, za utoaji wa huduma za tathmini ya makazi ya Serikali.
- Kuuza na kupangisha nyumba za Serikali kwa watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla.
- Kuwapangia nyumba za Serikali watumishi wa Umma.
- Uuzaji wa nyumba za Serikali kwa watumishi wa Umma kwa njia ya fedha taslimu au mkopo toka taasisi za fedha.
- Kupangisha nyumba za Serikali kibiashara.
- Kusimamia majengo ya Serikali na kuhifadhi kanzidata ya viwanja na majego ya Serikali.
- Kutoa huduma za usimamizi wa majengo ya Taasisi za Serikali (MDAs).
- Kutoa huduma ya usimamizi wa majengo na udalali.
Majengo ya Makazi yanayomilikiwa na TBA katika eneo la Magomeni Kota Awamu ya Pili.