Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Mfuko hautazalisha vitambulisho halisi. Wanufaika waliotimiza umri wa miaka 18 na wenye namba za NIDA watazitumia kupata huduma vituoni. Aidha kila mnufaika atapewa namba ya kitambulisho ambacho kitatolewa kama nakala tepe (soft copy) na kuitumia kupata huduma katika kituo kilichosajiliwa na Mfuko.
Ndiyo, kwa nyumba zinazojengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani au Ubia kati ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) au mikopo kutoka taasisi za kifedha hupangishwa au kuuzwa kwa wote, wasio Watumishi wa Umma na Watumishi wa Umma.  
Hapana, nyumba za Magomeni Kota haziuzwi. Zilijengwa mahususi kwa ajili ya wakaazi 644 waliokuwa wanaishi kwenye kota za zamani za Magomeni zilizokuwa na hali mbaya kabla ya kuvunjwa kupisha ujenzi wa nyumba bora na za kisasa.
Ofisi zetu za Makao Makuu zipo  Barabara ya Morogoro 13, Viwandani, Dodoma Tanzania na Ofisi ndogo za Makao Makuu zipo Barabara ya Sokoine 2, Dar es Salaam, Tanzania. Ofisi za Mikoa zinapatikana kwenye Yadi za Ujenzi katika mikoa yote Tanzania Bara.
Hapana, TBA haiwajengei nyumba Watumishi wa Umma na Wasio Watumishi wa Umma kwenye viwanja vyao. Kwa mujibu wa Sheria iliyoianzisha, TBA inatoa huduma ya makazi kwa Serikali, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla kwa kujenga kwenye maeneo yake pamoja na huduma za Ushauri na Ujenzi wa majengo ya S...