Nawezaje kupata nyumba ya kununua kwenye mradi wa Magomeni Kota?
Nawezaje kupata nyumba ya kununua kwenye mradi wa Magomeni Kota?
Mradi wa Magomeni Kota ni maalum kwa wananchi 644 waliokuwa wakaazi wa eneo hilo wakati nyumba zimebomolewa. Nyumba zile zilibomolewa kwa makubaliano ya kujenga nyumba mpya za kisasa kwa ajili ya kuwauuzia wananchi hao pekee, hivyo wananchi wengine wanashauriwa kuomba kupanga au kununua nyumba kwenye miradi mingine inayotekelezwa na Wakala.