Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi yatoa elimu sabasaba
Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi yatoa elimu sabasaba
Imewekwa: 06 Sep, 2023
Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, imeshiriki kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa – Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, wa Taasisi hiyo, Bw. Robert Manyama, ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa ya kuwepo kwa taasisi hiyo kuwasilisha malalamiko na taarifa za kodi kwa kufuata taratibu zilizopo.