Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAASISI YA USULUHISHI WA MALALAMIKO NA TAARIFA ZA KODI

"Haki na Usawa"

TOST yatabadilishana Uzoezi na Afrika ya Kusini

Imewekwa: 06 Sep, 2023
TOST yatabadilishana Uzoezi na Afrika ya Kusini

Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, imefanya ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini, kujifunza na kupata uzoefu wa namna bora ya kushughulikia malalamiko ya kodi kutoka kwa wananchi. Taasisi hiyo ilipata fursa ya kutembelea Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko ya Kodi nchini humo na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji.