ARCH. KONDORO AFUNGA KIKAO KAZI CHA MENEJIMENTI YA TBA
Menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeendelea na Kikao kazi kwa siku ya pili ambapo maada mbalimbali zimewasilishwa na kujadiliwa. Maada hizo zinajumuisha Taarifa ya Utendaji kazi ya Wakala kwa mwaka 2024/25, Mwongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2025/26, Mkakati wa Usimamizi na Uendelezaji wa Miliki pamoja na Hoja za Chama cha Wafanyakazi (TUGHE).
Akizungumza wakati wa kufunga Kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro amewashukuru wajumbe kwa utulivu na uchangiaji wenye tija pamoja na kuwasihi kutekeleza wajibu waliopewa wakati wa Kikao hicho kwa mustakabali wa maendeleo ya TBA.
Kikao kazi hicho kimefanyika kwa siku mbili (2) katika ukumbi wa mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 14 Januari, 2025.