Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

Imewekwa: 16 December, 2024
TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umefanya kikao na Rais wa Kituo cha Majengo kutoka Japan pamoja na ujumbe wake. Kikao hicho kimelenga kuonyesha fursa za uwekezaji kwenye eneo la uendelezaji wa Miliki ambapo TBA imefanya wasilisho la maeneo mahususi yaliyoandaliwa kwa ajili ya uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta Binafsi ya ndani na nje ya nchi.

Maeneo hayo yanajumuisha eneo la Canadian Masaki, Magomeni Kota, Temeke Kota jijini Dar es Salaam pamoja na eneo la Nzuguni B jijini Dodoma.