TBA YAPATA MAFUNZO YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA KATI YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI (PPP)
TBA YAPATA MAFUNZO YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA KATI YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI (PPP)
Imewekwa: 28 February, 2025

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepata mafunzo ya taratibu za Uwekezaji kwa njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Mafunzo hayo yametolewa na maafisa kutoka Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) ambao wametoa mafunzo ya utekelezaji wa miradi ya ubia inayohusisha Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Maafisa hao kutoka PPPC waliwasilisha mambo muhimu ya kuzingatia, majukumu ya wadau katika dhana ya PPP, njia za kuishirikisha sekta binafsi kwa mujibu wa sheria ya PPP pamoja na faida za PPP pindi taasisi ya Umma inapohitaji kuingia ubia na Sekta Binafsi katika Uwekezaji.
Mafunzo hayo yametolewa leo katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ndogo za TBA makao makuu jijini Dar es Salaam.