Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI WIZARA YA UJENZI.

Imewekwa: 16 December, 2024
WAZIRI ULEGA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI WIZARA YA UJENZI.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi katika Ofisi ndogo za Wakala ya Barabara (TANROADS), tarehe 11 Disemba 2024 Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour, pamoja na Wakuu wa Taasisi za Ujenzi.

Kikoa hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour, pamoja na Wakuu wa Taasisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa UFfundi na Umeme (TEMESA), Bodi ya Usajiri ya Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajiri ya Wakandarasi (CRB), Bodi ya Usajiri ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) NA Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT).

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Ulega amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu kumteua kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi. Aidha, Waziri Ulega ameahidi kuwapa ushirikiano Wakuu wa Taasisi hizo na kuendeleza yale yote ambayo yapo katika utekelezaji.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour amemkaribisha Waziri Ulega na kumuahidi ushirikiano kutoka kwa Menejimenti na watumishi wa Wizara pamoja na Taasisi zake.

Awali Mtendaji Mkuu TBA Arch. Daud Kondoro alitoa wasilisho kuhusu majukumu matatu yanayotekelezwa na TBA ambayo ni Usimamizi wa Miliki za Serikali, Utoaji wa huduma za Ushauri na Ujenzi wa Majengo ya Serikali. Vile vile, Arch. Kondoro ameelezea uhuhishaji wa Sheria ya Wakala wamepata ruksa ya kujenga na kuuza nyumba kwa umma.