Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Maadhimisho ya sabasaba

Imewekwa: 09 November, 2025
Maadhimisho ya sabasaba

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Prof. Geraldine Arbogast Rasheli atembelea mabanda ikiwemo banda la Wizara ya Fedha (@urtmof ), CMSA (@cmsa.go.tz ), SELF Microfinace (@self_mf ), IAA (@iaa_tz ) na TIA (@tia_tanzania ) katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba 2025 Jijini Dar es Salaam.

Lengo la ziara hii ni kukutana na wadau mbalimbali walioko kwenye mnyororo wa Ununuzi na Ugavi, kupokea maoni na mapendekezo ili kuboresha zaidi huduma za Wakala.

Maonesho haya yalianza 28 Juni,2025 na kutarajiwa kuhitimishwa 13 Julai,2025.