Uadilifu: Tunatumia viwango vya juu zaidi vya maadili vinavyoonyesha uaminifu na haki katika kila hatua tunayochukua.
Uwazi: Tunafanya kazi zetu kwa uwazi.
Uwajibikaji: Sisi kama watumishi wa umma tunawajibika kwa maamuzi na matendo yetu.
Ushirikiano: Tunafanya kazi pamoja, tunashirikishana uzoefu na kuheshimiana ili kufikia lengo letu la pamoja.
Ubunifu: Tunakumbatia utamaduni wa ubunifu katika nyanja zote na kujibadili kulingana na mienendo inayobadilika.
Utaalamu: Tunaonyesha kiwango cha juu zaidi cha uwezo na ufanisi tukiongozwa na tabia za kimaadili na miiko ya kitaalamu.
Kuzingatia Wateja: Tunajitahidi kutoa huduma bora ili kukidhi matarajio ya wateja.