Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Vigezo na Masharti

Masharti na Vigezo vifuatavyo vinasimamia matumizi yote ya Tovuti ya Wakala (Agency website) na tovuti zake za taarifa pamoja na maudhui yake yote yanayopatikana katika au kupitia tovuti yetu.
Huduma zetu hutolewa kwa kulingana na kukubali kwako bila marekebisho masharti na vigezo vyote vilivyomo humu, pamoja na sheria, sera, ilani, na taratibu zote zingine za uendeshaji ambazo zinaweza kuchapishwa mara kwa mara na Wakala.
Unakubali kwamba tunaweza kuboresha kiotomatiki tovuti pamoja na bidhaa na huduma zetu, na masharti haya yatahusika na maboresho yoyote. Tafadhali soma Mkataba huu kwa makini kabla ya kufikia au kutumia tovuti na huduma zetu. Kwa kufikia au kutumia sehemu yoyote ya maudhui na huduma za tovuti, unakubali kufungwa na masharti na vigezo vya mkataba huu. Iwapo hukubaliani na masharti na vigezo vyote vya mkataba huu, basi huruhusiwi kufikia au kutumia maudhui, bidhaa, na huduma zozote za tovuti.


Mabadiliko ya Masharti na Vigezo


Masharti na Vigezo vinaweza kubadilishwa wakati wowote bila taarifa. Nakala ya hivi karibuni ya Masharti na Vigezo vya Wakala itachapishwa hapa au inaweza kuombwa wakati wowote kwa kuwasiliana na GPSA.