Wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997, kama ilivyorekebishwa kwa Tangazo la Serikali Na.235 la tarehe 7 Desemba, 2007. Wakala ulizinduliwa rasmi tarehe 16, Juni 2008. Wakala una ofisi katika Mikoa yote 26 Tanzania Bara na uko chini ya Wizara ya Fedha.