JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi

Ninawezaje kupata cheti cha usajili wa uanachama?

Cheti cha usajili kinapatikana katika ofisi zetu za Dodoma. Hakikisha kuwa umelipa ada yako ya uanachama ya mwaka wa fedha husika.

Kwa waliopo nje ya Dodoma wanaweza kuomba kutumiwa kwa njia ya EMS. Utaratibu unaokuhitaji kujaza fomu na kulipia gharama ya 25,000/= ya kutumiwa (https://www.psptb.go.tz/pages/registration-forms?mid=70).

Kwa watakaohitaji kuchukulia katika ofisi za Dar Es Salaam wafike ofisi zetu zilizopo Keko au watume ujumbe wa Majina, Namba ya Usajili na Kategori  kwenda professionals@psptb.go.tz