MATOKEO YA MITIHANI YA 30 YA PSPTB
Wanafunzi 680 wafaulu mitihani ya PSPTB
Na Beatrice Sanga - PSPTB
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza matokeo ya mitihani ya 30 ya kitaaluma ya PSPTB iliyofanyika Mwezi May, 2025 katika vituo vinane nchini ikiwemo vituo saba Tanzania Bara na kituo kimoja kwa Tanzania Visiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi amesema kuwa watahiniwa 1506, walijisajili kwaajili ya mitihani hiyo huku waliofanya mitihani ni wanafunzi 1,421, wanafunzi 680 sawa na asilimia 47.9 wamefaulu kati ya watahiniwa 1,421 waliofanya mitihani ya kitaaluma, ilihali Watahiniwa 610 sawa na asilimia 42.9 wanarudia masomo yao na watahiniwa 131 sawa na asilimia 9.2 wamefeli na wataanza upya masomo yao katika ngazi husika.
Mbanyi amesema kuwa baadhi ya masomo yameonesha kufanywa vizuri na watahiniwa hii ikiwa ni ishara njema kwa taifa katika majadiliano ya biashara na ununuzi hususani katika mikataba ya kimataifa kama ambavyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza nchi kuwa na wajuzi wenye uwezo wa kufanya majadiliano yenye tija kwa taifa.
“Kwenye mitihani hii tulikuwa tunawapima pia somo mahususi la majadiliano ya kimikataba na wameonesha ujuzi wa kujaidiliana kwenye mikataba ya kimanunuzi na upimaji unaonesha kuwa watahiniwa sasa wanaanza kuiva vizuri kwenye eneo hilo, hii inaleta picha nzuri na faida kubwa kwa nchi yetu hasa katika kupata matokeo mazuri katika majadiliano ya biashara na mikataba ya kimanunuzi ambayo tunaingia kama nchi.” Amesisitiza Bwana Mbanyi.
Mbanyi amesema kuwa miongoni mwa masomo yaliyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo ni pamoja na Tendering Process and Techniques (D10), Business Consulting Skills (G09), Inventory Management (G13), Supply Chain Planning (G14), Strategic Supply Chain Management (C03), Business Negotiation (C05), Procurement Contract Management (C06), Global Strategic Procurement (C08), Leadership and Governance (C09), Strategic Asset Management (C10) na Procurement and Supply Chain Audit (C11) ili hali masomo ya Warehouse Operations (D01), Business Mathematics and Statistics (D03), Decision Making Techniques (G07), Asset Management (G10) na Financial Management (G11) hayakufanya vizuri..
Bodi imewapongeza wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani pamoja na wakufunzi kwa kuendelea kusimamia maadili na miongozo ya taaluma ya ununuzi na ugavi, huku pia ikitoa wito kwa wanafunzi ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao kuendelea na maandalizi kwaajili ya kujiandaa kwa awamu nyingine ya mitihani hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2025 huku ikiwaomba wanafunzi waliomaliza vyuo kujisaliji kwaajili ya kufanya mitihani hiyo.