Kurasimisha Biashara na Bidhaa
Shirika la Maendeleo ya Viwanda (SIDO) limekuwa likiwezesha Urasimishaji wa Biashara na Bidhaa kwa kuwaunganisha Wajasiriamali/Wanaviwanda na Mamlaka mbalimbali zinazorasimisha biashara kama ifuatavyo kama ifuatavyo:
Upatikanaji wa Leseni/Alama ya Uthibiti Ubora wa bidhaa
SIDO imekuwa na makubaliano maalumu na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kurahisisha upatikanaji wa nembo/leseni husika. Katika Makubaliano hayo Wajasiriamali/Wanaviwanda waliowekeza mtaji wa kuendeshea Biashara/bidhaa kati ya TZS 50,000.00 na TZS Milioni 75 ukiondoa gharama ya mtaji wa Ardhi na majengo watafaidika na mpango huu ambao unalenga kutoa leseni/Alama ya uthibiti ubora bila gharama yoyote. SIDO itahusika katika kufanya upembuzi wa awali, kushauri na kuelekeza na Kuhakikisha vigezo na masharti vilivyowekwa na TBS vinazingatiwa ili kupata nembo/leseni husika. SIDO baada ya Kukamilisha Mchakato wa upembuzi huo itawasilisha taarifa TBS ili hatua zinazofuata za urasimishaji kutekelezwa.
Upatikanaji wa Leseni za Biashara
Shirika lina shirikiana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutoa barua na vyeti vya Utambulisho ili Biashara zao ziweze kusajiliwa. Usajili huo unahusika na Majina ya Biashara/Kampuni (Business Names), Leseni za Biashara (Business License), Hati Miliki na Ataza (Copyrights) (Intellectual Property Rights) na Usajili wa Kampuni.
Pamoja na Mamlaka na Taasisi mbalimbali SIDO imekuwa ikiwezesha Wajasiriamali mbalimbali kufanya Usajili kama Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kulingana na bidhaa wanazozalisha au Biashara wanazofanya. Katika Urasmishaji bidhaa/Biashara SIDO imekuwa muhimili mkubwa sana katika Mchakato husika.

