SIDO imekuwa ikisaidia wajasiriamali wadogo na wa kati kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji rahisi wa vifungashio na huduma za ufungashaji. Nyenzo za ufungashaji zimezingatiwa kama mojawapo ya changamoto ambazo wajasiriamali hawa wamekuwa wanakumbana nazo. Hii ni kwa sababu ya idadi ndogo ya wazalishaji na wauzaji wa vifaa mbalimbali vya kufungasha kama vile chupa za ukubwa mbalimbali, vizipo vya chupa, seal, n.k
Hapa nchini Tanzania, ni wazi kuwa vifungashio ni muhimu sana katika sekta ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na masuala yote yanayohusiana na bidhaa za kilimo, viwanda, n.k. Uchaguzi wa vifaa vya kufungasha hutegemea aina ya bidhaa, mahitaji ya sekta, na masuala yote yanayohusu mazingira.
Ili kuwezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kupata nyenzo hizi muhimuza kufungasha, SIDO imeweza kukusanya maelezo mbalimbali ya viwanda vinavyozalisha vifungashio wakiwemo wasambazaji katika maeneo mbalimbali katika mikoa yetu. Hii itarahisisha upatikanaji wa vifungashio kwa karibu kulingana na bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali katika mkoa husika.
Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali wajasiriamali wanazozipata kwa kununua moja kwa moja kwa wazalishaji, SIDO imeanzisha kituo cha vifungashio na ufungashaji kwa lengo la kuweza kununua kwa wingi toka viwandani na kuweza kusambaza kupitia mikoa yetu iliyopo nchi nzima. Ifuatayo ni orodha ya wazalishaji na wasambazaji wa vifungashio mbalimbali kutoka kutoka katika baadhi ya mikoa. Pata kiambatisho cha orodha ya baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wa vifungashio

