Huduma za ushauri wa ki-ufundi

USHAURI WA KI-UFUNDI

SIDO, kupitia ofisi za mikoa na TDCs, inatoa huduma za ushauri wa kiufundi/teknolojia katika maeneo ya kuchagua teknolojia, upangaji wa mifumo ya uzalishaji viwandani, usalama na afya viwandani, utengenezaji na ukarabati wa mashine, utengenezaji wa bidhaa mpya, uzalishaji wa bidhaa bora, ufungaji wa mashine, uboreshaji wa mifumo ya uzalishaji, mwongozo wa jinsi ya kupata viwango na ubora wa bidhaa, n.k. Kazi hii inafanywa kwa kuwatembelea wateja mahali pa kazi na kuwashauri moja kwa moja pale wanapotembelea ofisi za SIDO.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo