SIDO hutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) kwa ajili ya kukuza mitaji ya miradi mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwa watu binafsi au vikundi kwenye sekta za biashara, uzalishaji pamoja na uwekezaji kwenye miundombinu ya biashara, zana na vifaa vya uzalishaji.
1. AINA YA MIFUKO NA UTOAJI WA MIKOPO:-
SIDO hutoa mikopo hadi shilingi milioni 5 kupitia mfuko wa kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) na hadi Shilingi milioni 6. 5 kupitia mfuko wa mzunguko wa mkoa (RRF). Pia SIDO kwa kushirikiana na benki ya CRDB PLC na Benki ya AZANIA LTD hutoa mikopo kuanzia shilingi milioni 7 hadi milioni 50, kupitia mfuko wa dhamana kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (Credit Guarantee Scheme) na kuanzia shilingi milioni 8 hadi milioni 500, kupitia mfuko wa SANVN (Viwanda Scheme)
A. Mikopo kupitia mfuko wa dhamana (CGS) hutolewa katika mikoa yote Tanzania Bara kupitia Benki ya CRDB PLC na SANVN (Viwanda Scheme) hutolewa katika mikoa yote Tanzania Bara kupitia Benki ya AZANIA LTD.
Kipindi cha marejesho ni kati ya miezi sita (6) hadi miaka mitatu kwa mfuko wa NEDF, RRF na CGS. Kipindi cha marejesho ni hadi miaka saba (7) kwa mfuko wa SANVIN.
B. Riba ya mkopo kwa mfuko wa NEDF ni asilimia 9 kwa mwaka kwa miradi ya uzalishaji na asilimia 12 kwa mwaka kwa miradi isiyo ya uzalishaji.
C. Riba ya mkopo kwa mfuko wa RRF ni asilimia 22 kwa mwaka kwa miradi ya uzalishaji.
D. Riba ya mkopo kwa mfuko wa Dhamana ni asilimia 9 kwa mwaka kwa miradi ya uchakataji wa mazao ya kilimo (Agro- Processing)
E. Riba ya mkopo kwa mfuko wa SANVIN ni asilimia 13 kwa mwaka kwa miradi ya sekta ya uzalishaji.
2. VIWANGO VYA MIKOPO
|
AINA YA MKOPO |
KIWANGO CHA CHINI (TSHS) |
KIWANGO CHA JUU (TSHS) |
SEKTA |
|
NEDF |
-
- |
1,000,000(Vikundi)
5,000,000 |
Biashara, huduma , nyinginezo Uzalishaji |
|
RRF |
- |
6,500,000 |
Uzalishaji |
|
CGS |
7,000,000 |
50,000,000 |
Uzalishaji wa mazao ya kilimo |
|
SANVIN |
8,000,000 |
500,000,000 |
Uzalishaji |
3. MASHARITI YA MIKOPO
Masharti ya mikopo hayatofautiani sana kati ya mfuko mmoja hadi mwingine. Lengo ni kumwezesha mjasiriamali kuweza kuwekeza na kumpatia mtaji wa kufanya biashara
Mikopo hutolewa kupitia ofisi za SIDO - Mkoa na mwombaji lazima awe ametimiza masharti yafuatayo;-
(a) Mwombaji lazima awe na umri usiopungua miaka 18 na awe raia wa Tanzania.
(b) Mradi unaoombewa mkopo lazima uwe unakubalika kisheria, umefanyiwa upembuzi yakinifu wa kifedha na unakubalika kijamii.
(c) Mradi lazima uwe umesajiliwa kisheria, mmiliki ana hati ya usajili wa jina la biashara na /au leseni halali ya biashara.
(d) Eneo la mradi liwe la kudumu na kutambulika na mamlaka za ndani.
(f) Mwombaji awe anatambulika kwa viongozi wa mtaa husika na viongozi hao waoneshe utayari wa kuthibitisha makazi na uwepo wake kwenye biashara husika.
(g) Mwombaji lazima awe na nia ya kulipa mkopo husika.
(h) Mwombaji lazima awe na Akaunti Benki yenye jina la biashara husika.
(i) Kwa mkopo wa mtu binafsi, mwombaji lazima awe na wadhamini pamoja na dhamana ya mkopo
(j) Kwa mikopo ya vikundi, waombaji lazima wawe tayari kuunda kikundi na kuweka akiba ya asilimia 20 ya thamani ya mkopo kama dhamana ya mkopo husika.
(k) Kwa mfuko wa dhamana, mwombaji lazima awe amewahi kukopa SIDO au kupata huduma nyingine kama vile teknolojia, mafunzo , masoko, ushauri wa kibiashara na ufundi au kupata huduma kupitia Programu mbalimbali zilizotekelezwa na SIDO kama vile MUVI KONGANO, KAIZEN n.k
(l) Kwa mfuko wa SANVIN waombaji wawe Wajasiriamali waliohudumiwa na SIDO
Kwa maelezo zaidi waweza kuwasiliana nasi
kupitia ofisi ya SIDO ya mkoa iliyokaribu nawe au
kupitia anwani yetu hapa chini

