Je nawezaje kujiunga na mfumo wa GIMIS?
Je nawezaje kujiunga na mfumo wa GIMIS?
Hatua ya kwanza, mteja atapaswa kujaza fomu maalum na kisha kuziwasilisha katika ofisi yoyote ya GPSA. Fomu hizi zinapatikana katika tovuti ya Wakala ya ‘www.gpsa.go.tz’ au kwa kutembelea ofisi/kituo chochote cha GPSA.
Hatua itakayofuata ni kufunguliwa akaunti yake na kisha kukabidhiwa nywila ili aweze kuingia katika mfumo wa utoaji huduma za GPSA kielektroniki wa “GPSA Integrated Management Information System-GIMIS” kupitia anuani ya “https://gimis.gpsa.go.tz/login” kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta.