Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Kwa nini Taasisi Nunuzi zinatangaza zabuni za vifaa na huduma ambazo zinatangazwa na kupatikana GPSA na hatua gani zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo?

Kwa mujibu wa Kanuni ya 127 (7) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 taasisi nunuzi haitatakiwa kuanzisha au kutangaza zabuni ambayo aidha vifaa au huduma husika inapatikana GPSA au vimewekewa utaratibu wa upatikanaji wake kupitia dirisha la Vifaa na Huduma Mtambuka (VHM) kwenye mfumo wa Ununuzi wa NeST. Aidha, ni muhimu kwa taasisi nunuzi kuzingatia kuwa Kanuni ya 125 (1) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 imeelekeza kuitisha zabuni za ushindani mdogo (mini-competition) pale tu vifaa au huduma husika itakuwa haipatikani GPSA kwa ushahidi wa cheti kitakachokuwa kimetolewa (Certificate of non-availability).