Ni Kwa namna gani wafanyabiashara na makampuni binafsi yananufaika na huduma za GPSA?
Ni Kwa namna gani wafanyabiashara na makampuni binafsi yananufaika na huduma za GPSA?
GPSA hununua vifaa na huduma kutoka kwa wafanyabiashara kwa njia ya uwazi na ushindani, hivyo fursa sawa hutolewa kwa wafanyabiashara wote. Aidha kupitia Ununuzi wa pamoja wa Vifaa na Huduma Mtambuka kupitia Mikataba Maalum, wafanyabiashara wanapata taarifa zote za zabuni na kushiriki kwenye zabuni kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma wa NeST unaopatikana kupitia anuani ya “www.nest.go.tz”. Utaratibu huu unawapunguzia wafanyabiashara gharama na muda wa kuzunguka kwenye kila taasisi.