Je mfumo wa Ununuzi wa kielektroniki wa NeST ni nini?
Je mfumo wa Ununuzi wa kielektroniki wa NeST ni nini?
NeST ambao ni ufupisho wa maneno ya Kiingereza ‘National e-Procurement System Tanzania’ ni mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma ambapo kwa sasa michakato yote ya Ununuzi wa Umma lazima ifanyike huko kutokana na maelekezo ya Serikali iliyoanza rasmi mwezi Julai, 2023 kwa taasisi zote za Umma ikiwemo GPSA.Mfumo huu huendeshwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma Serikalini (PPRA).
Hivyo basi washiriki wote wa Ununuzi wa Umma ikiwemo taasisi za Serikali pamoja na wazabuni wote ili waweze kushiriki ni lazima kujiunga kupitia tovuti ya ‘’www.nest.go.tz’’.