Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Utaratibu gani unatumika kwa wafanyabiashara kuingia kwenye orodha ya wazabuni wa kuuza Vifaa na Huduma Mtambuka (VHM) katika taasisi za Umma?

Kwa kuwa michakato yote ya Ununuzi wa Umma kwa sasa inafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki wa NeST, hivyo basi mzabuni yeyote atapaswa kujiunga na kufungua akaunti katika mfumo huu kupitia anuani ya ‘www.nest.go.tz’ na kisha kujisajili katika dirisha la wazabuni wa Vifaa na Huduma Mtambuka (VHM). Baada ya kukamilisha usajili, mzabuni ataweza kushiriki zabuni zote zinazotangazwa na Taasisi za Serikali katika mfumo huu unaoendeshwa na kusimamiwa na Wakala kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Usajili unafanyika muda wote katika mwaka.