Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Ni utaratibu gani hutumika kupata vifaa na huduma kutoka GPSA?

Wateja wanaweza kupata huduma za GPSA kidijitali kupitia mfumo wa kielektroniki wa “GPSA Integrated Management Information System-GIMIS” kwa anuani ya “https://gimis.gpsa.go.tz/login” popote ulipo kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta. Kupitia mfumo huu wateja wataweza kupata orodha na bei ya vifaa vinavyopatikana, kufanyia malipo na kupata stakabadhi na kisha kupata huduma katika vituo vyetu vilivyoko mikoa yote 26 na baadhi ya Wilaya za Kinondoni (Dar es Salaam), Dodoma Mjini (Mtumba-Dodoma), Kahama (Shinyanga) na Ileje (Songwe). Kupitia mfumo huu wateja wataweza kupata taarifa mbalimbali ikwemo fedha na mwenendo wa matumizi yake kwa muda wowote.