Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni nani?

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Na. 30 ya mwaka 1997 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 235 la tarehe 7 Desemba, 2007 na kufanyiwa marekebisho kupitia Gazeti la Serikali Na. 133 la tarehe 13 Aprili, 2012. Kuanzishwa kwa GPSA ni matokeo ya Programu za uboreshaji wa utendaji katika sekta ya umma yaani “Public Service Reforms Program-PSRP” ambapo katika maboresho hayo iliyokuwa ‘Bohari Kuu ya Serikali’ ilifutwa na baadhi ya majukumu yake yalichukuliwa na GPSA. Uzinduzi wa GPSA ulifanyika rasmi tarehe 16 Juni, 2008. GPSA iko chini ya Wizara ya Fedha, na ina ofisi na vituo vya mafuta katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.