Wakala Wa Huduma Ya Ununuzi Serikalini

"Ununuzi Unaozingatia Thamani"

Ni kwa nini GPSA hulipwa kwanza kabla ya kutoa huduma/vifaa tofauti na wazabuni wengine ambao hutoa huduma/vifaa na kisha kulipwa?

Malipo kufanyika kwanza ni mfumo wa kiudhibiti kwa kuiwezesha Serikali kutozalisha madeni na hivyo kuruhusu upatikanaji wa huduma kwa vifungu vya bajeti vinavyokuwa vimekasimiwa pamoja na fedha kuwa imepatikana. Kanuni ya 344 (5) (a) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 zimeweka takwa kwa taasisi nunuzi kuhakikisha zinapowasilisha maombi ya mahitaji ziwe zimekwishafanya malipo ambayo yatahakikiwa kabla ya huduma kutolewa. Lengo la utaratibu huo ni kuziwezesha taasisi zinazotoa huduma kama GPSA kuwa endelevu na kuziepusha katika madeni yasiyolipika yanayoweza kusababishwa na taasisi nunuzi.