Majukumu
Majukumu
Majukumu na Malengo ya Kuanzishwa kwa Mfuko wa Misitu Tanzania
Mfuko wa Misitu Tanzania umeanzishwa kwa ajili ya kutekeleza malengo na majukumu yaliyoainishwa katika kifungu cha 80 cha Sheria ya Misitu Sura 323 kama ifuatavyo:
- Kuwezesha uhamasishaji jamii kupitia elimu na mafunzo kuhusu umuhimu wa uhifadhi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali misitu;
- Kuwezesha na kugharamia uhifadhi, uendelezaji na usimamizi wa misitu kwa kutoa ruzuku kwa vikundi na wadau wengine wanaojihusisha na uhifadhi, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali misitu;
- Kukuza, kuendeleza na kugharamia utafiti kwa lengo la kuboresha uhifadhi, uendelezaji na usimamizi wa rasilimali misitu;
- Kusaidia na kuiwezesha Tanzania kunufaika na mipango na misaada ya kitaifa na kimataifa iliyopo kwa ajili ya kuhifadhi na kulinda bioanuwai na kuendeleza rasilimali misitu;
- Kusaidia na kuwezesha vikundi na watu binafsi kushiriki katika mijadala na midahalo inayohusu misitu na kuandaa tathmini za kimazingira kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 18 cha Sheria ya Misitu Sura 323;
- Kusaidia na kuwezesha vikundi na watu binafsi ili wafuate Sheria ya Misitu, kanuni na miongozo husika; na
- Kugharamia shughuli nyingine zinazoendana na majukumu ya Mfuko na shughuli zinazohusiana na madhumuni ya Sheria ya Misitu Sura 323.