Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umeanzishwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Sheria ya Misitu Sura 323 kwa lengo la kuwa chanzo cha uhakika na endelevu cha fedha kwa ajili ya kuwezesha na kugharamia uhifadhi, usimamizi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali misitu hapa nchini. Mfuko huu unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini na shughuli za kila siku zinafanywa na Sekretarieti ya Mfuko.
Bofya ili Kupakua Tangazo la Kuitisha Maandiko ya Kuomba Ruzuku 2024
Maeneo ya kipaumbele ya kufadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania ni yale yanayolenga kuhifadhi na kusimamia misitu kwa uendelevu. Kwa kuzingatia majadiliano na wahojiwa pamoja na mapitio ya nyaraka mbalimbali hususan Sera ya Taifa ya Misitu, masuala yanayopaswa kushughulikiwa ni pamoja na usimamizi wa ardhi ya misitu ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mazao na huduma kwa kudumisha eneo la misitu la kutosha chini ya usimamizi madhubuti; kuimarisha viwanda na mazao ya misitu; kuhakikisha uhifadhi na usimamizi wa mfumo ikolojia pamoja na kuongeza uwezo wa kitaifa wa kusimamia na kuendeleza sekta ya misitu kwa kushirikiana na wadau wengine.
Soma zaidiMfuko wa Misitu Tanzania unatoa aina nne za ruzuku ambazo ni; ruzuku ndogo, ruzuku ya kati, ruzuku kubwa, na ruzuku za makusudi maalum. Makundi haya ya ruzuku yanatofautishwa kwa kiasi cha fedha zinazotolewa, walengwa wanaostahili, muda wa utekelezaji wa mradi na mchango katika ulinzi, uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya misitu. Aina za ruzuku zimefafanuliwa hapa chini kama ifuatavyo: 1. Ruzuku Ndogo (Kiasi kisichozidi Shilingi za Tanzania (TZS) milioni 10), 2. Ruzuku ya Kati (Kiasi cha zaidi ya TZS 10 milioni lakini kisichozidi TZS 20 milioni), 3. Ruzuku Kubwa (Kiasi cha zaidi ya TZS 20 milioni lakini kisichozidi TZS 50 milioni), 4. Ruzuku kwa Madhumuni Maalum (Kiasi kinachozidi TZS 50 milioni).
Soma zaidiMfuko wa Misitu Tanzania hufanya uperembaji wa miradi iliyopatiwa ruzuku. Zoezi la uperembaji uliofa...
Mafunzo ya kwa wanufaika wapya wa ruzuku kuhusu utaratibu wa kutekeleza miradi na usimamizi wa ruzuk...
TaFF yasaini mkataba wa utekelezaji wa Grant na mnufaika