Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA

Watu Binafsi

Watu binafsi wanaweza kuomba ruzuku ndogo ya kiasi cha fedha kisichozidi shilingi Milioni Tano (TZS 5,000,000/=) kwa ajili ya miradi ya upandaji miti au utafiti kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya misitu au ufugaji nyuki. Aidha, watawasilisha maandiko yaliyoandaliwa kwa kufuata muundo unaotolewa kila mwaka tangazo la kuomba ruzuku linapotangazwa.

i) Barua ya udhamini kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Kata anapoishi mwombaji wa ruzuku (kwa watu binafsi ambao sio wanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu);
ii) Barua ya udhamini kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji mradi utakapotekelezwa (kwa watu binafsi ambao sio wanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu);

iii)Barua ya udhamini kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri mradi utakapotekelezwa (kwa watu binafsi ambao sio wanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu);

iv) Muhtasari wa kikao cha familia kinachoonesha jinsi mradi unaoombewa ruzuku utakavyotekelezwa or fedha iliyotolewa itakavyorejeshwa iwapo mwombaji wa ruzuku atafikwa na umauti au kuwa kwenye hali yoyote itakayomfanya kushindwa kuendelea na utekelezaji wa mradi kama vile maradhi (kwa watu binafsi ambao sio wanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu);
v) Kitambulisho cha kuthibitisha uraia wa mwombaji wa ruzuku;
vi) Uthibitisho wa umiliki wa ardhi (muhtasari wa kikao cha familia kwa ardhi iliyopatikana kutokana na mgawo wa familia, hati miliki au hati miliki za kimila, mkataba au hati ya mauziano ya ardhi, barua na muhtasari kutoka Serikali ya Kijiji kwa waliopatiwa ardhi na vijiji), kwa miradi ya upandaji miti;
vii) Uthibitisho wa kudahiliwa kutoka Chuo husika kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu;
viii) Barua kutoka Kurugenzi inayohusika na udahili wa shahada za uzamili na uzamivu kuthibitisha kuwa mwombaji wa ruzuku amedahiliwa kwa ajili ya shahada husika;
ix) Barua kutoka kwa Mkuu wa Idara ya utambulisho na udhamini wa mwanafunzi wa shahada ya uzamili au uzamivu ambayo itathibitisha pia kuwa hana chanzo kingine cha fedha kwa ajili ya kugharamia utafiti wa masomo yake; na
x) Kwa miradi inayohusisha ununuzi wa vifaa na/au vitendea kazi waombaji wawasilishe vidadisi bei (quotation);