Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA

Tafiti

Taasisi za mafunzo na Taasisi za utafiti zinaweza kuomba ruzuku ya kati na ruzuku kubwa. Aidha, Taasisi za mafunzo na Taasisi za utafiti za Serikali zinaweza kuomba pia ruzuku maalum. Waombaji watawasilisha maandiko ya kuomba ruzuku yaliyoandaliwa kwa kufuata muundo unaotolewa kila mwaka tangazo la kuomba ruzuku linapotangazwa.

i) Barua ya utambulisho na udhamini kutoka kwa Mkuu wa Taasisi iwapo mwombaji ni Idara au Kituo;
ii) Muhtasari wa kikao cha Menejimenti au kikao cha Bodi kilichoketi na kupitisha andiko la mradi, na muhtasari huo usainiwe na wahusika;

iii) Uthibitisho wa umiliki wa ardhi (hati miliki, mkataba au hati ya mauziano ya ardhi, barua na muhtasari kutoka Serikali ya Kijiji kwa Taasisi ya mafunzo au Taasisi ya utafiti iliyopatiwa ardhi na vijiji), kwa miradi ya upandaji miti;
iv) Kibali cha kuruhusiwa kufanya shughuli za ufugaji nyuki ndani ya misitu ya hifadhi au maeneo mengine yaliyohifadhiwa (kwa miradi ya ufugaji nyuki) endapo utekelezaji wa mradi utafanyika nje ya eneo linalomilikiwa na Taasisi husika; na
v) Kwa miradi yote inayohusika na ujenzi waombaji wa ruzuku wanapaswa kuwasilisha michoro na mchanganuo wa gharama (BoQ). Aidha, kwa miradi ya ununuzi wa vifaa na/au vitendea kazi waombaji wawasilishe vidadisi bei (quotation).