Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA

Taasisi

Taasisi za Serikali zinajumuisha Mashirika, Mamlaka, Taasisi na Wakala wa Serikali; Mamlaka za Serikali za Mitaa; na shule za msingi na sekondari. Taasisi za Serikali zinaweza kuomba ruzuku ya kati, ruzuku kubwa na ruzuku maalum isipokuwa shule za msingi na sekondari ambazo zinaweza kuomba ruzuku ndogo. Aidha, ruzuku maalum inapaswa kuombwa na Mkuu wa Taasisi tu. Waombaji wa ruzuku watawasilisha maandiko ya kuomba ruzuku yaliyoandaliwa kwa kufuata muundo unaotolewa kila mwaka tangazo la kuomba ruzuku linapotangazwa.

Andiko la kuomba ruzuku linatakiwa kuambatana na vielelezo vifuatavyo:

i) Barua ya utambulisho na udhamini kutoka kwa Mkuu wa Taasisi iwapo mwombaji ni Idara au Kituo;
ii) Kwa Taasisi ambazo zina ofisi za wilaya, kanda na Taifa, maombi ya ruzuku ya kati na ruzuku kubwa yatakayowasilishwa kutoka wilayani yatapitishwa katika ngazi ya kanda;
iii) Shule za msingi na sekondari zinapaswa kuwasilisha barua ya udhamini kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ilipo shule husika;
iv) Uthibitisho wa umiliki wa ardhi (hati miliki, mkataba au hati ya mauziano ya ardhi, barua na muhtasari kutoka Serikali ya Kijiji kwa Taasisi ya Serikali iliyopatiwa ardhi na vijiji), kwa miradi ya upandaji miti;
v) Kibali cha kuruhusiwa kufanya shughuli za ufugaji nyuki ndani ya misitu ya hifadhi au maeneo mengine yaliyohifadhiwa (kwa miradi ya ufugaji nyuki) endapo utekelezaji wa mradi utafanyika nje ya eneo linalomilikiwa na Taasisi husika; na
vi) Kwa miradi yote inayohusika na ujenzi waombaji wa ruzuku wanapaswa kuwasilisha michoro na BoQ. Aidha, kwa miradi ya ununuzi wa vifaa na/au vitendea kazi waombaji wawasilishe vidadisi bei (quotation).