Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MFUKO WA MISITU TANZANIA

Kutoa Ruzuku

Imewekwa: 12 January, 2023
Kutoa Ruzuku
Mfuko wa Misitu Tanzania unatoa aina nne za ruzuku ambazo ni; ruzuku ndogo, ruzuku ya kati, ruzuku kubwa, na ruzuku za makusudi maalum. Makundi haya ya ruzuku yanatofautishwa kwa kiasi cha fedha zinazotolewa, walengwa wanaostahili, muda wa utekelezaji wa mradi na mchango katika ulinzi, uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya misitu. Aina za ruzuku zimefafanuliwa hapa chini kama ifuatavyo:

1. Ruzuku Ndogo (Kiasi kisichozidi Shilingi za Tanzania (TZS) milioni 10),
2. Ruzuku ya Kati (Kiasi cha zaidi ya TZS 10 milioni lakini kisichozidi TZS 20 milioni),
3. Ruzuku Kubwa (Kiasi cha zaidi ya TZS 20 milioni lakini kisichozidi TZS 50 milioni),
4. Ruzuku kwa Madhumuni Maalum (Kiasi kinachozidi TZS 50 milioni).