Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Bodi ya Maziwa Tanzania

TDB Logo
​TCB YAAHIDI KUVIJENGEA UWEZO VIKUNDI VYA WAFUGAJI DODOMA
04 Apr, 2023
​TCB YAAHIDI KUVIJENGEA UWEZO VIKUNDI VYA WAFUGAJI DODOMA

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kupitia Mkurugenzi wake wa tawi la Dodoma Bw. Edward Mlowo imeahidi kushirikiana na Bodi ya Maziwa Tanzania katika kuvijengea uwezo vikundi vya wafugaji jijini Dodoma ili waweze kuanza kufuga kibiashara na kuona faida ya ufugaji wao.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa benki hiyo alipokutana na Maafisa Uzalishaji Maziwa toka Bodi ya Maziwa Tanzania alipowaalika ofisini kwake na kufanya nao mazungumzo mafupi kujadili namna watakavyoshirikiana katika kuvijengea uwezo vikundi hivyo na kuwapa mafunzo ya elimu ya kifedha kwa vikundi hivyo na hatimaye kutoa mikopo kwa vikundi vitakavyokidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.

Akielezea namna alivyoguswa na kikundi cha wafugaji "TUUNGANE GROUP" kilichopo Kata ya Mkonze jijini Dodoma kinavyoendesha shughuli zao za ufugaji ameona kuna haja taasisi za kifedha kuwawezesha vikundi kama hivyo ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya ufugaji.

Kwa upande wa Bodi ya Maziwa Tanzania imeahidi kuendelea kuwaunganisha wadau wake na TCB iliwaendelee kupata huduma za mikopo na kujengewa uwezo kutoka benki hiyo.