Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Bodi ya Maziwa Tanzania

TDB Logo
Huduma za Usimamizi wa Sheria

Huduma za Usimamizi wa Sheria

 

Bodi ya Maziwa inafanya kazi za Usimamizi wa Sheria katika nyanja tano nazo ni ;

 

1. Usajili wa Wadau

 

Hii ni tathmini ya mahitaji ya wadau wa maziwa ambayo hufanywa kulingana na sheria ya maziwa sehemu ya 17 (1) ambayo inahitaji mtu yeyote anayehusika na maziwa na bidhaa za maziwa kusajiliwa na Bodi

 

2. Ukaguzi wa maziwa na bidhaa za maziwa

Hii hufanywa mara kwa mara ili kuhakikisha maziwa yanahifadhiwa katika hali ya usafi ili kuhakikisha ubora na usalama wa maziwa kwa watumiaji

 

3. Kufuatilia ubora wa maziwa na bidhaa za maziwa

 

Bodi inaendelea kufuatilia ubora wa maziwa na bidhaa za maziwa katika mnyororo wa thamani ya maziwa. Hii inasaidia kutoa taarifa zitakazosaidia kupanga na kufanya maamuzi juu ya namna ya kulinda afya za watumiaji wa maziwa Tanzania

 

4. Kupitia na kuangalia viwango vya maziwa

 

Bodi ni mwanachama wa kamati ya Ufundi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambayo inapitia na kuangalia viwango vya maziwa na bidhaa za maziwa nchini ili kulinda afya za watumiaji wa maziwa na bidhaa za maziwa

 

5. Usimamizi wa maziwa na bidhaa za maziwa zinazoingia na kutoka nje ya nchi

Bodi ya Maziwa inasimamia uingizaji na utoaji wa maziwa na bidhaa za maziwa kwa kutoa vibali vya kuingiza/kutoa maziwa ndani ya nchi. Hii inasaidia kuongeza masoko ya maziwa na bidhaa za maziwa zinazotengenezwa nchini Tanzania