BILIONI 24.4 KUFANIK...
BILIONI 24.4 KUFANIKISHA HUDUMA YA MAJISAFI TINDE- SHELUI
24 Jan, 2023
BILIONI 24.4 KUFANIKISHA HUDUMA YA MAJISAFI TINDE- SHELUI

Mhe. Jumaa Aweso akabidhi fedha kiasi cha shilingi Bilioni 24.4 kwa ajili ya kuhakikisha Mradi wa Majisafi wa Tinde- Shelui unakamilika na mwisho wakaazi wote wa maeneo hayo kupata majisafi na salama kwa ajili ya matumizi kijamii, kiuchumi na kibiashara. Aidha amewataka wananchi wote wa maeneo yanayopitiwa na mradi huo  kuhakikisha wanatunza miundombinu ya maji ambayo ni Matenki, Mabomba na Viungio vyake.