RAIS SAMIA AWASILI W...
RAIS SAMIA AWASILI WINDHOEK NCHINI NAMIBIA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA TROIKA PLUS
08 May, 2023
RAIS SAMIA AWASILI WINDHOEK NCHINI NAMIBIA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA TROIKA PLUS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC) tarehe 07 Mei, 2023. Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).