Logo ya COPRA yazinduliwa kwenye kikao cha wawekezaji
19 Dec, 2023
Tukio la uzinduzi wa logo mpya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Regulatory Authority - COPRA), Logo hiyo imezinduliwa kwenye mkutano wa pamoja ambapo pichani waliopo ni Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene Mlola na Bodi ya COPRA.
Uzinduzi na Mkutano huo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wawekezaji wa Ndani katika Sekta ya Kilimo tarehe 18 Desemba 2023, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.