Ajenda za Utafiti
Agenda kuu ya Kitaifa ya Utafiti ni nyenzo muhimu inayotoa dira inayowaongoza
Watafiti katika kupanga na kutekeleza miradi ya kitafiti kwa kuzingatia mahitaji ya wadau
wa sekta ya mifugo. Agenda kuu ya kitaifa ya Utafiti ilitayarishwa kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali ambapo walianisha vipaumbele muhimu saba (7) kama ifuatavyo:
- Uboreshaji Mbari za Mifugo
- Uboreshaji wa Malisho na vyakula vya Mifugo
- Uimarishaji wa Afya ya Mifugo
- Uimarishaji wa masuala ya Kiuchumi, kijamii na kitamaduni
- Utafiti katika Mifugo ilisiyozoeleka
- Utafiti wa masuala mtambuka, na
- Uongezewaji wa Thamani kwa mazao ya mifugo
Vipaumbele vilivyoainishwa kwenye agenda kuu ya kitaifa ya Utafiti wa Mifugo vimezingatia
matumizi sahihi wa teknolojia na bunifu mbalimbali ili kufikia malengo tarajiwa ya kuongeza tija
ya uzalishaji mifugo