Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Wanyama Wadogo Wanaocheua

Taasisi imekuwa ikifanya utafiti wa wanyama wadogo wanaocheua ambao ni Mbuzi na Kondoo kama ifuatavyo

1. Utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa Kondoo aina ya Kondoo Wekundu wa Kamasai na Kondoo wa Persia mwenye Kichwa Cheusi (BHP)

Lengo ni la mradi huu ni kuwahifadhi na kuwaendeleza kwa kuchagua kondoo bora kwa ajili ya kuendeleza kizazi chao na wale wasiofaa wanaondolewa. Tunataka kuwa na kondoo wa asili wenye uzito mkubwa, wanaokuwa kwa haraka,wanaozaliana kwa haraka na wanaovumilia magonjwa na maazingira magumu hivyo kupunguza idadi ya vifo.

2. Utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa Mbuzi bora aina ya Malya

Lengo ni kuendeleza Mbuzi bora na wakipekee ambae ni matokeo ya utafiti uliofanyika hapa Tanzania kwa kuunganisha Mbuzi wa asili na mbuzi wengine kutoka Afrika Kusini na Pakistani. Mbuzi hawa wameongeza uwezo wa mbuzi huyo wa kuzaliana kwa haraka, kuwa na uzito mkubwa unaofikia kilo 80, uwezo wa kukua haraka na huvumilia mazingira magumu na hata magonjwa. Mbuzi hawa bora huhifadhiwa na kuendelezwa kwa lengo la kuzalisha kwa wingi na kusambaza kwa wafugaji ili kuboresha Mbuzi wa asili.

3. Utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa mbuzi wa asili

Lengo ni kuendeleza mbuzi wa asili kwa kuzalisha na kuchagua mbuzi bora kwa ajili ya kuendeleza kizazi chao na wale wasiofanya vizuri huondolewa. Mbuzi wa asili licha ya kuwa na umbo dogo wanapendwa sana katika nchi za mashariki ya kati hasa wale wanaopatikana maeneo ya wilaya ya Iramba mkoani Singida. Kwa kuwa soko la mbuzi hawa lipo, Taasisi inaendelea kuwahifadhi na kuwachagua kwa lengo la kupata mbuzi wanaozaliana kwa haraka hasa wenye uwezo wa kuzaa mapacha, wanaokuwa waraka, wanaovumilia ukame, mazingira magumu, magonjwa na uwezo wa kujitaftia chakula wenyewe. Utafiti huu unalenga kutafta namna bora ya kuimarisha afya za wanyama hawa ambao wamekuwa wakiathiriwa sana na magonjwa ya homa ya mapafu na mengineyo kwa kuimarisha chanjo na kutafta tiba za magonjwa hayo.

4. Utafifi wa mbuzi bora wa maziwa aina ya Tanga

Lengo ni kuendeleza mbuzi wa kisasa ili wa maziwa kwa kuunganisha mbari  za kisasa za mbuzi wa maziwa ambao ni Toggenburg, Saanen na Norwegian wanaounganishwa na mbuzi wa asili waliochaguliwa wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi, kuzaa kwa haraka, kukua haraka na kuzaa mapacha.Tunatarajia kuzalisha mbuzi wa maziwa aina ya Tanga atakayeweza kuzalisha maziwa ya kutosha katika mazingira ya joto kali, ukame na mazingira magumu ya malisho yanayopatikana maeneo mengi ya Tanzania. Tunatarajia kuwa na mbuzi mwenye uwezo wa kutoa lita tatu (3) kwa siku ambaye atasambazwa kwa wafugaji wadogo wadogo ili kuinua kipato chao na kuimarisha afya ya familia hasa kupambana na tatizo la utapiamulo linalowakumba watoto wengi nchini Tanzania kutokana na kukosa maziwa ya kutosha.