Misingi Mikuu
Katika kutekeleza majukumu na kazi zake, TALIRI itazingatia misingi mikuu yafuatayo:
Uadilifu: Maadili ya hali ya juu, nidhamu ya kazi na heshima.
Utaalamu: Kuwa na wafanyakazi wenye sifa stahiki katika utoaji huduma.
Ukarimu: Uundaji wa mazingira rafiki na umakini wa hali ya juu kwa matarajio ya mteja.
Uwajibikaji na Wajibu: Wajibu wa kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Kutanguliza Mahitaji ya Mteja: Kutoa huduma kwa kutanguliza mahitaji ya mteja.
Kujielekeza Kupata Matokeo: kujitahidi kutimiza malengo yanayotarajiwa katika kutekeleza majukumu na wajibu.
Uwazi: Uwazi katika shughuli za TALIRI na
Kutopendelea: Utoaji wa huduma bila ubaguzi (fursa sawa kwa wote)