Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
Ng'ombe wa Maziwa

Tunauza mitamba ya ng'ombe bora wa maziwa ifuatayo:

1. Aina ya Holstein Friesian wanapatikana katika kituo cha TALIRI Uyole (Mbeya) kilichopo Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini.

2. Chotara wenye mchanganyiko wa Zebu, Borani, Ayrshire, Jersey, Friesian na Girolando waliofanyiwa utafiti katika kituo cha TALIRI Tanga kanda ya Mashariki ambao ni maalumu kwa wafugaji waliopo kanda ya Pwani.

3. Mpwapwa wenye sifa ya kuzalisha maziwa ya kutosha na nyama bora katika mazingira magumu yenye ukame na ukosefu wa malisho wa mikoa ya Kanda ya Kati kama Dodoma na Singida na baadhi ya maeneo ya kanda ya Ziwa na Kasikazini. Wanapatikana kituo cha Mpwapwa Kanda ya Kati, Mabuki Kanda ya Ziwa na West Kilimanjaro Kanda ya Kasikazini.

4. Chotara wa Borani na Ayrshire wanapatikana TALIRI Naliendele Kanda ya Kusini ambao wanafaa kwa wafugaji waliopo mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na maeneo mengine yanayofanana na hali ya hewa kama ya mikoa hiyo.