Huduma za Ushauri
TALIRI hutoa huduma za ushauri kwa wafugaji wanaotembelea vituo vya Taasisi kujifunza au kupitia programu zake za kutembelea wafugaji katika mashamba yao. Pia huduma hizi zinapatikana kupitia mawasiliano ya namba za simu, barua pepe na kurasa za mitandao ya kijamii. Huduma hizi ni bure kwa ushauri wa awali na endapo mfugaji ataomba watalaamu kufika shambani kwake atagharamia gharama za usafiri na huduma kwa watalaamu hao kwa kadri itakavyoonekana inafaa.