Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
TALIRI Kanda ya Magharibi

TALIRI KANDA YA MAGHARIBI

  1. Historia fupi ya kanda

Kanda ya Magharibi inajumuisha mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora na Kigoma imeanza  rasmi Jula1 2023.   TALIRI Kanda ya Magharibi ina ofisi yake ya Kanda katika Halmashauri ya  Nsimbo Mkoani Katavi na inatumia majengo ya zamani yaliyokua yanatumiwa na Halmashauri hiyo. TALIRI Kanda ya Magharibi ina eneo lenye ukubwa wa ekari 1042 kwa ajili ya shughuli za utafiti  wa mifugo. Kanda hii ipo kimkakati kwa ajili ya kutoa huduma za utafiti, ushauri na uhaulishaji wa teknolojia za uzalishaji mifugo na mbegu bora za malisho katika Mikoa ya Magharibi. Wafugaji wa kanda ya Magharibi hufuga ng’ombe wa asili aina ya Ankole na Tarime, na hutegemea  malisho asili ambayo hayadumu kwa kipindi kirefu. TALIRI Kanda ya Magharibi imejipanga kuzalisha malisho na mbegu bora hii itapunguza uhaba wa malisho ya mifugo  na kuongeza tija kwenye ufugaji.  Hii itapunguza wafugaji kuhamahama na kusababisha migogoro  na watumiaji wengine wa ardhi.   

  1. Miradi kwa utafiti

Miradi mingine itakayotekelezwa na TALIRI Kanda ya Magharibi ni kama ifuatavyo;

a)        Utafiti na uzalishaji wa Ng‘ombe bora wa Nyama;

b)        Utafiti na uzalishaji wa Ngombe bora wa Maziwa;

c)         Utafiti na Uzalishaji wa Mbuzi na Kondoo

d)        Utafiti na uzalishaji wa ndege wafugwao (kuku)

  1. Vituo vya kanda

Kwa sasa Kanda ina kituo kimoja ambacho kipo katika Halmashauri ya Nsimbo na ndio makao makuu ya Kanda.

  1. Vituo tarajiwa

TALIRI Kanda ya Magharibi imejipanga kuongeza maeneo mengine ya kitafiti katika mikoa ya Rukwa, Kigoma na Tabora ili kufikisha huduma karibu na wafugaji na wadau wengine wa mifugo.