DKT. FADHILI GUNI AKIWA KATIKA JUKUMU LA KUWAJENGA UWEZO VIJANA (YOUTH PEACE CLUBS)
28 Feb, 2024
Baadhi ya Watafiti kutoka TALIRI Kanda ya Kusini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kanda, Dkt. Fadhili Guni wakiwa katika jukumu la kuwajenga uwezo vijana (Youth Peace Clubs) wa kata mbili za Michenjele na Mihambwe wilayani Tandahimba juu ya ufugaji bora wa kuku na baadae watapewa kuku na kujengewa mabanda. Mradi huu unafadhiliwa na #undptz na kuratibiwa na #GPF chini ya mradi wa Dumisha Amani na Kutekelezwa na TALIRI.
Lengo la mradi huu ni kuzuia vijana kujihusisha/ kujiunga na makundi ya kihalifu kwa kukosa shughuli za kuwaingizia kipato. Mradi huu unatekelezwa kwenye wilaya za #Mtwara, #Tandahimba, #Nachingwea, #Tunduru na #Nyasa