Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania

TALIRI Logo
DR. ANDREW CHOTA AKIWA NA MKURUGENZI WA KANDA YA MASHARIKI WAKIKAGUA ZOEZI LA UVUNAJI WA MALISHO NA UFUNGAJI WA MABUNDA YA HEI KATIKA KITUO CHA TALIRI TANGA.
28 Feb, 2024
DR. ANDREW CHOTA AKIWA NA MKURUGENZI WA KANDA YA MASHARIKI WAKIKAGUA ZOEZI LA UVUNAJI WA MALISHO NA UFUNGAJI WA MABUNDA YA HEI KATIKA KITUO CHA TALIRI TANGA.

Mkurugenzi wa Utafiti Dr. Andrew Chota akiwa na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki wakikagua zoezi la uvunaji wa malisho na ufungaji wa mabunda ya hei katika kituo cha TALIRI Tanga, kilichopo mkoani Tanga katika kanda ya Mashariki.

ikumbukwe malisho hayo yaliyooteshwa wakati wa mvua za vuli zilizopita na uvunaji unaendelea kabla ya mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwezi ujao. Zoezi la upandaji na uhudumiaji wa shamba hili ulishirikisha wafugaji kutoka wilaya ya Muheza, Tanga-Tanzania na walijifunza hatua kwa hatua. Pia tuliwashirikisha wafugaji wote kupitia mitandao ya kijamii.

Malisho haya yanavunwa na kufungwa kwenye mabunda ya hei yenye uzito kati ya kilo 20-25 na yanaweza kuuzwa wastani wa TZS 5,000/= na kuongeza kipato cha mfugaji.